Inaendelea....
Nikiwa kwenye gari mida ya jioni, simu yangu ilianza kuita kwa jazba, ndipo nilipoipokea. Ilikuw namba ngeni,
MIMI; "hallo!, nani mwenzangu"
SIMU; Akajibu " ni mimi kurusumu "
MIMI; Nilijikuta najibu kwa hamu " Naaam, kurusumu, Umempata kaka yako?"
KURUSUMU; Akajibu " mmmh!, haikuwa rahisi kaka yangu kila mtu ninayemuuliza anasema hamjui, yaan mpaka nachanganyikiwa"
MIMI; "pole na uchovu wa kumtafuta kaka yako kurusumu"
KURUSUMU; "Asanteeee"
MIMI; " Uko maeneo gani nikuijie?"
KURUSUMU; "Nilipanda daladala, niko kituo cha daladala mawasiliano"
MIMI; "Siko mbali na maeneo hayo ngoja hapo nije nikuchukue nikupeleke nyumbani sawaaaa mama?"
KURUSUMU; " Sawaaaa nakusubiria kaka"
Nikageuza gari tayari kumfuata kurusumu katika kituo cha daladala mawasiliano,
BAADA YA DAKIKA KUMI NA TANO
MIMI; (baada ya kuangaza kwa muda nikamuona kurusumu) "Naona umenisubiri weeee! Mpaka umefloti (umechoka)"
KURUSUMU; Akajibu huku akitabasamu "yaani, we acha tu kila mtu ananishangaa maana nikasema au ndio ameghairi kuniijia huku, mbona ntakoma mimi"
MIMI; " Hapana, nisingeweza kufanya hivyo dada yangu, (huku nikifungua mlango wa tax yangu) "ingia ndani nikupeleke nyumbani ukapumzike"
NILIMPELEKA KURUSUMU NYUMBANI NA KISHA NIKARUDI KIJIWENI KWANGU NIZIDI KUTAFUTA MKATE WA KILA SIKU.
Baada ya masaa 6 mbele ilikuwa kama saa 5 na nusu usiku, nilikuwa nawasili nyumbani kwangu, nikapaki gari kwa jirani yangu ambaye ndiye bosi wangu anayeitwa MZEE KIVIKO na kisha kuelekea kwangu.
MIMI; " hodi (nikipiga mlango) nifungulie kurusumu mimi kaka yako"
KURUSUMU; (baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa " karibu kaka, samahani nimechelewa kufungua mlango"
MIMI; " Usijali kurusumu (huku nikimtazama kwa furaha)
SIKU HIYO NDIO NILIPOUONA UREMBO WA BINTI KURUSUMU JINSI MUUMBA ALIVYOSHUGHULIKA KULIDIZAINI UMBO LAKE LA NYIGU, USIKU HUO ALIKUWA KAJIFUNGA KANGA (LUBEGA)
KURUSUMU; (Akaniandalia chakula mezani) karibu kaka chakula" (huku akitabasamu)
MIMI; " Asante kurusumu, sikudhani kama utajiongeza kupika maana nina njaaa! We acha tu"
KURUSUMU; Aking'ata vidole " Usijali kaka niliona kwamba nikusaidie kupika"
MIMI; SIKU HIYO CHAKULA NILIONA KITAMU SANA AMBACHO SIJAWAHI KULA TANGU NIZALIWE JAPO ILIKUWA UGALI DAGAA " chakula leo kitamu! Kweli"
KURUSUMU; Kwa aibu " Asante kaka"
KURUSUMU; Ukimaliza kula kuna maji ya moto nimekutengea utaenda kuoga upunguze uchovu"
MIMI; " Asante sana kurusumu maana nilivyolowa jasho hili mmmh! Ni siri yangu tu"
KURUSUMU; Akawa anatiza video......
MIMI; Macho yangu yalizidi kumtazama uzuri wake uliojaa ukarimu ndani yake, " Asante kwa chakula nimeshiba kweli"
KURUSUMU; "Aaasantee! Kushukuru, pia na we asante kwa kuhemea vyakula"
Basi tulipongezana kwa muda kisha nikaenda kuoga na kuukosha mwili wabgu ulojaa uchovu kila mahali.
USIKU ULIPOFIKA NILIOTA NDOTO YA AJABU SANA,
Itaendelea.....jumatatu
Usisahau kusubscribe ili uwe wa kwanza kupata taarifa juu ya kinachofuatia.
0 Maoni