Tulipofika tegeta kwa kaka yake, nilikaribishwa kwa furaha sana,
KAKA KURUSUMU; "Asante sana ndugu kwa kumsaidia dada yangu, amenieleza kisa chote mpaka ulipokutana naye na kumsaidia, Je, ugapenda nikupe zawadi gani?
MIMI; (nikicheka kwa haya) "nilimsaidia bila kuja kutaka malipo nashukuru mungu tu amekupata kaka yake salama"
KAKA KURUSUMU; "Basi sawa sitksahau wema wako kwa dada yangu"
TULIPATA CHAKULA CHA MCHANA KISHA NIKAAGA NA KUONDOKA, KIUKWELI KAKA WA KURUSUMU ALIKUWA NI TAJIRI SANA VILE NILIVYOKUWA NIMETARAJIA.
BAADA YA MASAA 2 KUPITA NA HEKAHEKA ZA JAM (FOLENI) NJIANI HATIMAYE NILIFIKA KITUONI UBUNGO NA KUENDELEA NA KAZI YANGU YA UDEREVA.
DMB; "Naona jembe langu umerudi mzigoni, yaani muda tu ulikuwa hoi sa hivi unacheka na una nguvu? Kweli mzungu mchawi hayo madawa ulopewa hospitali ni balaa!
MIMI; " Acha uswahili jembe piga kazi bwana"
DMB; " haya bwana mzee mi yangu macho tu"
SIKU HIYO NILIKUWA NA BAHATI YA AJABU NILIPIGA KAZI MPAKA SAA 6 USIKU NA KUPATA PESA NZURI AMBAYO SIKUWAHI PATA TANGU NIANZE KAZI YA UDEREVA.
NA ILIPOFIKA SAA 6 NA NUSU NILIWASIRI NYUMBANI KWANGU, PEMBENI YA NYUMBA NIKAONA PAKA NA MBWA WANAPIGANA NA PAKA ALIKUWA KAUMIZWA VIBAYA NILIMUONEA HURUMA SANA, NIKAMFUKUZA YULE MBWA NA AKATOKOMEA GIZANI. NILIPOKUWA NAINGIA NDANI YULE PAKA AKANIFATA NYUMA AKITAKA TUINGIE NAYE NDANI, NIKAMFUKUZA LAKINI HAKUONDOKA, NILIAMUA KUINGIA NDANI NA KUFUNGA MLANGO.
MIMI; nilipoamka asubuhi nilistaajabu kuona yule paka yuko nje akiwa kajilaza pembeni ya ngazi ya mlango, nilipika chai na baadaye nikampelekea chakula kiasi yule paka na nikamuacha akila chakula,
NILIPOINGIA NDANI GHAFLA KWA NYUMA NIKASIKIA ASANTE, NILIPOGEUKA NIKAMUONA PAKA AKIWA MBALI ANAONDOKA NIKABAKI NAJIULIZA NI NANI ALIYESEMA ASANTE,
Itaendelea........
0 Maoni