Nikasimamisha gari yangu mbele kidogo, Nilipotoka nje ya gari nikaonaona vidume vitatu vinajiandaa kumbaka yule dada huku mmoja kati ya wale wanaume kashika kisu mkono wa kulia,
Nikatoa sauti kali ya kiume "Nasema mwacheni huyo dada (nikarudia kusema mara mbili)
Mwanaume mmoja; akasema, " We kama nani wazungumza?" huku akinifata na kisu mkononi,
Nikajiandaa kwa kukabiliana nae kwa lolote,
Aliponisogelea nikampiga ngumi ya kifua, alipojaribu kunichoma kisu nikamkunja mkono na kumnyang'anya kile kisu, kiukweli nilikuwa vizuri hasa katika mapigano,
Wale wanaume wenzake wawili walivyoona kipigo nilichompa mwenzao hawakuthubutu kunisogelea walikacha kwa mbio kali,
Nikamuuliza dada unaitwa nani? Na mbona uko mazingira haya?
Yule dada akasema "naitwa kurusumu na hapa nilikuwa namtafuta kaka yangu anayeishi hapa dar es salaam nimemtafuta bila mafanikio na sijui niende wapi"
Nikamwambia " pole sana dada yangu lakini utawezaje kumtafuta mtu dar es salaam bila mawasiliano? Ni jambo gumu sana hasa hapa jijini hapa.
Kurusumu; "nilikuwa nayo mawasiliano lakini nilipofika ubungo simu yangu niliibiwa"
Mimi; "pole sana dada yangu, ila kama hutojali twende kwangu ukalale leo na kesho ikifika uendelee kumtafuta ndugu yako"
Kurusumu: kwa kusitasita akasema "sa..sa.saawaa."
Nikamchukua kurusumu na kupanda naye katika gari yangu kisha kwenda naye nyumbani kwangu.
Tulipofika nyumbani kwangu nilikuwa nina nyumba ndogo tu yenye vyumba viwili na sebule, hivyo nilimpatia chumba kimoja ili aweze kujipumzisha.
Mimi; "ukihitaji kuoga maji yako hapa kwenye pipa na bafu lipo hapo mlango wa kwanza katika korido"
Kurusumu; "sawa nashukuru"
Ilipofika asubuhi kurusumu aliamka na kunikuta nimeshapika chai na vitafuna,
MIMI; Karibu chai dada, inaonekana ulikuwa na uchovu mkubwa kwa pilikapilika za jana"
KURUSUMU; "Asante kaka"
MIMI; "Unatokea mkoa gani"
KURUSUMU; "Nimetokea mkoa wa Tabora, Wilaya ya nzega"
MIMI; "Kaka yako alisema anaishi maeneo gani hapa jijini?"
KURUSUMU; Akajibu "Tegeta"
MIMI; Nkajibu "Tegeta ni kubwa ila usikate tamaa ntakupeleka Tegeta ukamtafute kaka yako na ukimkosa unakaribishwa kwangu tena mpaka utakapompata" guku nikitoa noti ya elfu 10 na kumpatia Kurusumu,
KURUSUMU; "Asante kaka, nashukuru"
Tulikunywa chai na tulipomaliza nilimpeleka kurusumu mpaka Tegeta ili aweze kumtafuta kaka yake, nikampatia namba yangu ya simu kama tahadhari pindi akimkosa ndugu yake, Nikaondoka kuelekea kijiweni kwa sababu Mimi nilikuwa Dereva wa Tax hapa jijini,
Itaendelea......Jumapili
0 Maoni